Habari

VIONGOZI NA WAKUU WA TAASISI WAMESISITIZWA KUSIMAMIA UWAJIBIKAJI.

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais katiba Sheria, Utumishi na Utawala bora Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema ni jukumu la wakuu wa Taasisi na vitengo kukaa pamoja kujadili namna ya kuwaelimisha Watendaji wao juu ya utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma.

VIJANA NA WANAFUNZI WAMETAKIWA KUTUMIA VYEMA MITANDAO YA KIJAMII

Naibu Waziri wa maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Anna Athanas Paul  amewasisitiza  Vijana na Wanafunzi Kutojirikodi na kujirusha katika Mitandao ya Kijamii  ili kujiepusha na Matatizo yatakayo jitokeza.

Akizungumza katika Madhimisho ya Siku ya Familia Duniani Naibu Waziri huyo amesema ili kulinda Maadili na Malezi bora kwa Watoto ni vyema kwa Wazazi kuwasimamia Watoto pamoja na kuwasisitiza Vijana  kuacha Tabia za  kujituma katika Mitandao ya Kijamii na badala yake kuitumia kwa kuwaletea Faida.

ASKARI JKU WAMEHIMIZWA UWAJIBIKAJI NA UFANISI

Mkuu wa Jeshi la kujenga Uchumi (JKU), Kanal Makame Abdallah Daima, amewataka Wafanyakazi wa Jeshi hilo kufanyakazi kwa bidii na Ufanisi, kwa lengo la kuisaidia Serikali katika kuimarisha Uchumi.

Mkuu huyo wa JKU ameyasema  hayo Chuo cha Uongozi JKU Dunga wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Jeshi hilo kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo ikiwa ni muendelezo wa kukumbushana kuhimizana  Majukumu yao ya Kazi ya kila siku ndani ya Jeshi hilo.

WANANCHI WAMETAKIWA KUPIMA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Wanawake wenye umri kuanzia Miaka 18 hadi 69 wametakiwa kujitokeza kwenye upimaji wa Saratani ya shingo ya Kizazi katika Hospitali ya Mnazi Unguja Mmoja na Chakechake Kisiwani Pemba

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Amour Mohamed Suleiman alipokuwa akizungumza na Timu ya Madaktari kutoka China wanaotarajiwa kuanza zoezi la upimaji wa Saratani ya shingo ya Kizazi hapa Zanzibar.

NCHI ZA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI KUSHIRIKIANA KATIKA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA HALI YA HEWA

    Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),Mhe. Jaji Mshibe Ali Bakari ametoa rai kwa wataalamu kutoka nchi za Kanda ya Afrika Mashariki kuboresha ushirikiano ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza hususani kipindi cha matukio ya hali mbaya ya hewa.

     Mhe. Mshibe alisema hayo wakati akifungua rasmi Mkutano wa Kamati ya Usimamizi wa Programu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ya Utabiri wa Hali Mbaya ya Hewa kwa nchi Wanachama Kanda ya Afrika Mashariki, unaofanyika Dar es Salaam, 14-17 Mei, 2024.

TANZANIA KUNUFAIKA NA UANACHAMA KATIKA JUMUIYA ZA NISHATI ZA AFRIKA MASHARIKI

   Tanzania inatarajiwa kunufaika na uanachama wake katika jumuiya za nishati za Afrika Mashariki yaani (East African Power Pool) na Kusini (South Africa Power Pool) katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara ya umeme pamoja na kuunganishwa katika gridi ya pamoja.

DKT.MWINYI ASIFU FURSA ZA BIASHARA BAINA YA ZANZIBAR NA COMORO

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar na Comoro zina Mahusiano maalum ya kuchanganya damu wa kindugu hivyo ameridhia kufunguliwa kwa Konseli Mkuu wa Comoro hapa Zanzibar.

     Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Comoro Mhe.Saidi Yakubu aliyefika kumuaga baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Ikulu Zanzibar tarehe 14 Mei 2024.

SERIKALI YATAMBUA UMUHIMU WA UTAFITI KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA MAENDELEO

    Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu na mchango wa utafiti wa kisayansi katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kisayansi zinazochangia kuchochea maendeleo ya nchi.

CHINA NA TANZANIA KUSHIRIKIANA KATIKA HUDUMA ZA MAKUBUMBUSHO

    Makumbusho ya Taifa ya China na Tanzania zimekubaliana kushirikiana katika kubadilishana uzoefu, teknolojia na kuwa na maonesho ya pamoja kwa lengo la kuhakikisha kuwa huduma za makumbusho zinakuwa na faida kwa pande zote mbili za nchi hizo.

    Makubaliano hayo yamefikiwa katika mazungumzo kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la China, Gazo Zheng yaliyofanyika kwenye Makumbusho ya China jijini Beijing Mei 14,2024.

ZAIDI YA WANANCHI ELFU 40 HALMASHAURI YA MTAMA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA

   Zaidi ya wananchi Elfu 40 kutoka katika Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi wanatarajiwa kunufaika na mradi wa Maji na usafi wa mazingira unatekelezwa  na taasisi isiyo ya kiserikali ya 'Heart to Heart' chini ya ufadhili wa Shirika la Kimataifa la KOICA utakaoghalimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.6

    Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo katibu tawala Mkoa wa Lindi Bi zuwena Omary amewahimiza wananchi na taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya Mkoa huo kutunza na kulinda vyanzo vya maji ili viendelee kutoa ya maji kwa  kwa muda mrefu.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.