Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Amekihakikishia Chama Cha Mawakili Zanzibar Kuwa Serikali Inathamini Na Kuunga Mkono Kazi Nzuri Inayofanywa Na Chama Hicho Ya Kuwasaidia Wananchi Katika Masuala Ya Kisheria.
Rais Dkt. Mwinyi Ameyasema Hayo Alipokutana Na Uongozi Wa Chama Cha Mawakili Zanzibar Ulioongozwa Na Rais Wa Chama Hicho, Wakili Joseph Shaban Magazi, Waliofika Ikulu, Zanzibar.
Akizungumzia Suala La Uwekezaji Lililowasilishwa Na Chama Hicho Kwa Kuomba Kupatiwa Eneo, Rais Dkt. Mwinyi Ameitaka Taasisi Hiyo Kulifanyia Tathmini Ya Kina Suala Hilo Na Kujipanga Vema Kabla Serikali Haijafanya Maamuzi Ya Kuwapatia Eneo La Ardhi, Ili Kuepuka Kukaa Muda Mrefu Bila Kufanyiwa Uwekezaji.
Rais Wa Chama Cha Mawakili Zanzibar, Joseph Shaban Magazi, Amempongeza Rais Dkt. Mwinyi Kwa Uongozi Wake Na Juhudi Zake Katika Kuifungua Zanzibar Na Kuifanya Kuwa Kituo Bora Cha Uwekezaji Kwa Nchi Za Afrika Mashariki Na Kati.
Rais Dkt. Mwinyi Ametumia Fursa Hiyo Kuikabidhi Gari Taasisi Hiyo, Ambayo Iliomba Katika Maadhimisho Ya Siku Ya Sheria Yaliyopita, Kwa Ajili Ya Utekelezaji Wa Majukumu Yake.
