HARAKATI ZA KUKITAMBUA KISWAHILI MITANDAONI ZAANZA

MHE.PAUL MAKONDA
English

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Paul Makonda, amesema Serikali imeanza mazungumzo na UNESCO pamoja na Uongozi wa Kampuni Mama inayomiliki Mitandao ya Kijamii ya Faceebok, Instagram na Whatsapp (Meta) ili lugha ya Kiswahili itambulike rasmi kwenye majukwaa ya Mitandao hiyo na kuwezesha Vijana wanaotengeneza maudhui kwa Lugha hiyo walipwe malipo makubwa kulingana na kazi zao.

Makonda ameyazungumza haya wakati wa Kongamano la 5 la Idhaa za kKswahili Duniani lililofanyika Jana Arusha.

Makonda anasema licha ya Maudhui ya Lugha ya Kiswahili hususani ya Tanzania kuwa mazuri na kupata Watazamaji wengi lakini warushaji maudhui hayo Wanalipwa kidogo kutokana na lugha hiyo kutokuwa rasmi kwenye majukwaa ya Mitandao hiyo ukilinganisha na Lugha ya Kiingereza

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.