Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Ameushauri Uongozi Wa Kituo Cha Tafiti Za Kiuchumi, Kijamii Na Uchambuzi Wa Sera Zanzibar –Zrcp- Kuandaa Mikutano Na Mijadala Na Wadau Ili Kuwaelimisha Kuhusu Umuhimu Wa Kutumia Matokeo Ya Tafiti Katika Utekelezaji Wa Majukumu Yao.
Ni Ziara Ya Ujumbe Wa Kituo Cha Tafiti Za Kiuchumi, Kijamii Na Uchambuzi Wa Sera Zanzibar –Zrcp- Katika Ikulu Ya Vuga Hapa Zanzibar.
Mkurugenzi Wa Zrcp Juma Reli Na Ujumbe Wake Wamefika Kupata Fikra Pevu Za Mheshimiwa Rais Wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi.
Pamoja Na Ushauri Wa Zrcp Wa Kuandaa Mikutano Na Mijadala Na Wadau, Rais Dkt Hussein Mwinyi Amezungumzia Umuhimu Wa Kufanya Maboresho Katika Mifumo Ya Usajili Wa Malipo Ya Kidijitali Ili Kuongeza Uwazi Na Kurahisisha Muda Hususan Katika Sekta Ya Umma Na Kushauri Kuangaliwa Upya Kwa Sera, Sheria, Na Kanuni Katika Eneo Hilo.
Mkurugenzi Mkuu Wa Zrcp Juma Hassan Reli Amekubaliana Na Mapendekezo Ya Rais Dkt Mwinyi Na Kwamba Kituo Kipo Tayari Kushirikiana Na Serikali Kutoa Tafiti Na Mapendekezo Yatakayochangia Maboresho Ya Mifumo Ya Malipo Ya Kidijitali, Ikiwa Ni Pamoja Na Kusaidia Mapitio Ya Sera, Sheria, Na Kanuni Ili Kuimarisha Uwazi Na Ufanisi Katika Sekta Ya Umma
