Wito Umetolewa Kwa Taasisi Binafsi Kushirikiana Vyema Na Taasisi Za Elimu Pamoja Na Kuekeza Katika Tafiti Hususan Za Kisayansi Na Teknolojia Kuhimiza Ubunifu Katika Ufundishaji Na Ujifunzaji Ili Kuinua Viwango Vya Tafiti Na Ubora Wa Elimu.
Wito Huo Umetolewa Jijini Dar Es Salaam Na Makamu Wa Rais Wa
Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe Dkt. Emmanuel Nchimbi Wakati Akizungumza Katika Uzinduzi Wa Mashirikiano Ya Pamoja Kati Ya Waajiri Na Vyuo Ambapo Amesema Kupitia Mpango Huo Sekta Binafsi Inaweza Kuchangia Maendeleo Ya Nchi Kwa Kufadhili Tafiti Na Ufadhili Wa Wanafunzi Kwa Fani Mbambali Ili Kukidhi Soko La Ajira
Kwa Upande Wake Waziri Wa Elimu Sayansi Na Technolojia Mhe. Pro. Adolf Mkenda Amesema Mpango Huu Ulikua Ni Ahadi Ya Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hasaan Kukamilika Ndani Ya Siku 100 Baada Ya Kuapishwa Kwake Ili Ukatimizwe Kikamilifu Na Kuleta Matunda Mema Kwa Jamii.
Nao Wadau Wa Sekta Binafsi Na Baadhi Ya Wamiliki Wa Viwanda Wamesema Kuwa Mpango Huu Unatekelezeka Na Utakuwa Na Tija Kwa Jamii, Na Hapa Wanaeleza Mchango Wao Katika Kuwajengea Uzoefu Na Kuwapa Mafunzo Vijana
