Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) imefanikiwa kutatua mgogoro wa mpaka kati ya vijiji viwili uliyodumu zaidi ya miaka kumi huko Wilaya Kisarawe Mkoani Pwani.
Kijiji cha Kibuta ni miongoni mwa Vijiji nane ambavyo, Mipango ya Matumizi ya Ardhi imetekeleza katika Wilaya ya Kisarawe, na Mgogoro huo ambao ulikuwa kati ya kijiji cha Kibuta na Kijiji cha Mloo uliodumu zaidi ya miaka kumi umepatiwa majibu baada ya tume hiyo kupima na kutafsiri ramani ya mipaka ya asili ya vijiji hivyo. Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kibuta akiwemo Diwani wa kata ya Kibuta wameishukuru Serikali kwa kuja na mpango huo kwani mbali na Kutatua Mgogoro huo pia vijiji hivyo vinane vimepimwa na kupangiwa matumizi ikiwemo miundo mbinu ya elimu afya na barabara.
"Kupitia hawa wawezeshaji kwenye mpango bora wa Matumizi ya Ardhi, kwenye huu Mgogoro kati ya Kijiji cha Kibuta na Kijiji cha Mlao Mgogoro umeisha tunamshukuru Rais wetu Mama Samia kupitia wataalam wetu" alisema Diwani wa kata ya Kibuta Mariam Abasi.
Msimamizi wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi Wilaya ya Kisarawe Kutoka tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi
Bwn. Edward Mpanda Ameeleza mwitikio wananchi wa vijiji hivyo ni namna gani walivyojitokeza kuunga mkono zoezi hilo pamoja na kueleza na namna walivyotekeleza hadi kuupitisha mipango hiyo katika mikutano ya vijiji.
"Wananchi wengi walikuwa hawajui Mipaka ya vijiji, na sisi kama tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi tunao wataalam wetu lakini pia tumechukua wapima Ardhi ngazi ya Wilaya na Mkoa, wao kama wataalam wamechukua michoro na kuanza kuichakata lakini kwa kutumia hizi timu za kuhakikisha maslahi ya mipaka kwa wananchi tumeingia nao site na kuanza kutafuta mawe qmbayo yalikuwa yameshapandwa na baadhi ya mawe tumeibua na tukaweka, lakini kwenye vile Viijiji ambavyo vimeibuka mfano hiki Cha Kibuta ambacho kiligawanywa kikapatikana Kijiji cha Mloo ilibidi tushirikishane na wanakijiji tukaweka mpaka ambao umeweza kutenganisha" Alisema Edward Mpanda Msimamizi wa Mipango ya Mtumizi ya Ardhi Wilaya ya Ardhi Kisarawe.
Vijiji vilivyotekelezewa Mipango hiyo itayodumu kwa miaka 10 na kupitishwa katika mikutano ya vijiji katika wilaya ya Kisarawe ni Kibuta,Chang’ombe ‘A’, Mengwa, Msegamo Chale, Bembeza, Boga, na Ngongele.
