SERIKALI YASAINI MKATABA UJENZI HOSPITALI YA MKOA MAHONDA

UTIAJI SAINI UJENZI HOSPITAL
English

 Wizara ya Afya Zanzibar imetiliana Saini Mkataba wa Ujenzi wa Hospital ya Mkoa Mahonda na Kampuni Cross World Construction Limited.

Akizungumza baada ya Utaji Saini Mkataba huo Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar Dkt. Saada Mkuya Salum amesema Mradi huo utakua ufumbuzi wa upatikanaji wa huduma za Kibingwa za Afya na kuipunguzia gharama Serikali ya kusafirisha Wagonjwa kutoka Nje ya Nchi.

 Akitoa maelezo kuhusu Ujenzi wa Mradi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt.  Mngereza Mzee Miraji Hospitali hiyo itakua ya Ghorofa Tano, na kutoa huduma mbalimbali za Kibingwa kwa Ngazi ya Mkoa.

 Nae Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Cross World Instruction Limited Ndg.Himid Iddi Mgeni Amesema Mradi huo ni wa Miezi 18 unatarajiwa kukamilika kwa Wakati ili kutimiza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuimarisha huduma za Afya kwa Wananchi Mijini na Vijijini.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.