Kwa mara ya kwanza katika historia ya Zanzibar imezindua Matangazo ya Utalii katika Jiji la London Nchini Uingereza kwa kubandika Matangazo yanayosomeka Tembelea Zanzibar kwenye Mabasi maarufu ya Abiria yanayoitwa London Buses. Hatimaye historia imeandikwa.
Mabango makubwa yanayochagiza, kushajihisha na kuuvutia Utalii wa Zanzibar yameanza kuonekana Leo kwenye Mabasi ya Abira maarufu kama London Luses Nchini Uingereza.
Uzinduzi wa Kampeni hii umefanyiika Leo Jijini London na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Ndg. Mbelwa Kairuki ndiye aliyefanya kazi hiyo.
Kamisheni ya Utalii Nchini inasema lengo lake ni kuvitangaza Vivutio vya Utalii vya Zanzibar katika Jiji la London ambalo linapokea Watalii Milioni 20 kwa Mwaka.
Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Arif Abbas Manji anasema lengo la Kamisheni ni Zanzibar kufikia idadi kama ya London ya Utalii.
Ikumbukwe Nchi za Bara Ulaya zinachangia Asilimia 68 ya Watalii Wanaoitembelea Zanzibar.
Kutoka London Mtanzania Anayeishi na kufanya kazi Nchini Uingereza Dkt. Leah Mwainyekule Anasema hii ni fursa ya kipekee kwa Zanzibar kujitangaza katika moja ya Masoko makubwa Barani Ulaya.
Kwa mujibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar ubunifu huu wa kujitangaza haujawahi kutokea katika Historia ya Zanzibar na lengo ni kuwafikia Watalii wengi zaidi kwa gharama nafuu zaidi.
