WANASWA KWA KUHUJUMU MRADI WA MAJI WA MIJI 28
WATU wanne wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tabora kwa tuhuma za kuhujumu Mradi wa Maji wa Miji 28 unaoendelea kutekelezwa na serikali katika Wilaya za Sikonge, Urambo na Kaliua ili kumaliza kero ya wananchi.
Kaimu Kamanda wa Polisi ACP Constatine Mbogambi amethibitisha kukamatwa watuhumiwa hao wakiwa na vifaa mbalimbali vilivyoibiwa kwenye mradi huo Wilayani Urambo. Akitaja baadhi ya vifaa vilivyokamatwa kuwa ni mashine kubwa 3 za kuchomelea mabomba, grenda mashine 2 za kukatia mabomba, nyaya 9 za kuunganishia grenda hizo na lita 40 za mafuta ya mitambo ya hydroliki.
