WATU WENYE ULEMAVU WAHIMIZWA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

CHAMA CHA MAPINDUZI

Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Simiyu, kimewahimiza Watu wenye Ulemavu na wazee kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura, ili wapate haki ya kuchagua Viongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo wa Simiyu, Shemsa Mohamed, wakati akihutubia Viongozi wanaotokana na Chama hicho Tarafa ya Ngulyati, katika ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa ya kusikiliza Kero za Wananchi na kuzitafutia majawabu.

Amehimiza pia upendo na mshikamano kwa viongozi wa Chama hicho Tawala.

M/kiti wa CCM Mkoa Simiyu.Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Saimon Simalenga, akizungumza kwenye Kikao hicho cha Viongozi wanaotokana na chama cha Mapinduzi Tarafa ya Ngulyati, amepiga marufuku wanufaika wa fedha za mpango wa kunusuru kaya masikini Tasaf, kukata kwa ajili ya kuchangia Ujenzi wa Miradi ya maendeleo.

Wakala wa Maji safi na usafi wa mazingira Wilaya ya Bariadi Ruwasa, imewahakikishia Wananchi uptikanaji wa Maji safi karibu na maeneo yao.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.