UJENZI OFISI ZA MASHEHA KUONGEZA UWAJIBIKAJI

Ujenzi wa ofisi za Masheha

      Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe.Masoud Ali Mohammed, amesema Ujenzi wa Ofisi za Masheha katika Shehia itawawezesha kuongezeka uwajibikaji na Wananchi kuwa huru pindi wanapofata huduma.

   Akitembelea Ujenzi wa Ofisi ya Sheha Shehia ya Ijitimai Mwanakwerekwe, amemtaka Mkandarasi wa Ujenzi huo Kikosi cha KVZ kuharakisha Ujenzi huo ili kuwawezesha Masheha kuongeza ufanisi wa kiutendaji kwa Wakaazi wao.

     Mkuu wa Wilaya ya Magharib 'b', Hamida Mussa Khamis, amesema anamatarajio  kwa Masheha kuleta mabadiliko na kuwaondoshea  mazingira magumu ya kazi waliyokumbana nayo hapo kabla. 

     Mkandarasi wa Ujenzi huo Mkuu wa Kikosi cha Valantia KVZ, Luten Kanal Said Ali Shamhuna, amesema Ujenzi huo umezingatia kiwango cha ubora kinachosimamiwa na Wakala wa Majengo Zba na kuahidi kukamilika kwa wakati uliopangwa.

      Nae Sheha wa Shehia  ya Ijitimai Rashid  Mwadini Omar, pamoja na Mwananchi wa Shehia hiyo wamepongeza hatua ya Serikali kuwajengea Ofisi ambazo zitaleta ufanisi na usiri wa kazi, tofauti na hapo awali.

     Jumla ya Ofisi 388 zinatarajiwa kujengwa kwa kila Wilaya za Unguja na Pemba .

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.