SERIKALI KUTOA POSHO LA NAULI NA KUIMARISHA POSHO LA LIKIZO.

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshiwa Dr Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha mazingira bora ya Wafanyakazi  kwa kutoa Posho la nauli la kila Mwezi kwa wanaostahiki  pamoja na  kuboresha Posho la  likizo  kwa Wafanyakazi  Nchini

Ameyasema hayo huko Uwanja wa Michezo Gombani katika maadhimisho ya kumbukumbu ya   Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika Kitaifa Kisiwani Pemba

Mheshimiwa Rais amesema ili kupatikana kwa ufanisi unaotokana  na azma ya utekelezaji huo  ni wajibu kwa Wafanyakazi kutekeleza majukumu yao kwa  bidii  umoja na uwajibikaji  katika sehemu zao za  kazi

Aidha aimetaka Wizara ya kazi kukaa pamoja na Shirikisho la Vyama vya  Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) kila robo ya Mwaka ili kuzungumza na kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya Wafanyakazi pamoja na kuangalia namna bora ya kuwaletea wafanyakazi maslahi na haki stahiki

Akisoma risala ya Wafanyakazi katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya  Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) Khamis Mwinyi Moh'd amesema Waajiri na Waajiriwa watakuwa na kazi kubwa katika kufikia uwajibikaji makazini iwapo hakutakuwepo majadiliano ya pande zote za Kiutendaji.

Naye Waziri wa kazi uchumi na uwekezaji Zanzibar Mheshimiwa Sharif Ali Sharif amesema Wizara itahakikisha inasimamia vyema haki na wajibu wa Waajiri na Waajiriwa ili kuondosha lawama na malalamiko ambayo yanazorotesha kasi ya utendaji kazi

Kaulimbiu ya Mei Mosi Mwaka huu ni kuimarika kwa maslahi na mazingira ya kazi ni msingi wa ufanisi kazini

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.