MKURUGENZI SAZANI AWATAKA WANAFUNZI KUYAFANYIA KAZI MAFUNZO YA STADI ZA MAISHA

SAZANI

     Wanafunzi wametakiwa kuyafanyia kazi kwa vitendo Mafunzo ya Stadi za Maisha wanapokuwa katika mazingira ya Skuli na Nje ya Skuli kwa kubuni vitu mbali mbali ambavyo vitawasaidia katika maisha yao ya baadae.

   Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sazani Zanzibar Ndg.Safia Mkubwa Abdallah mara baada ya kutoa Mafunzo ya Stadi za Maisha kwa Wanafunzi, yaliyofanyika huko  Skuli ya Sekondari Fidel Castro Chake Chake Pemba.

    Amesema Mafunzo hayo yana lengo la kuwajenga Wanafunzi kuzitumia stadi za maisha kwa kuanzisha miradi tofauti yatakayoweza kuwasaidia wao  na Jamii inayowazungunguka.

   Aidha amesema kutokana na ushindani mkubwa wa Soko la Ajira linaloikumba Dunia Mafunzo hayo yatawaisaidia kubuni vitu vipya vya tofauti mbali na kujivunia kupata ufaulu mzuri wa Kimasomo kama ilivo zoeleka.

    Akizungumzia changamoto ya ukosefu wa Elimu ya Stadi za Maisha kwa Wananfunzi Mwalimu Maryam Amour Khamisi amesema ipo haja kwa Wanafunzi kupewa Elimu hiyo ili kujitambua na kuwa wabunifu.

    Nao baadhi ya Wanafunzi wa Skuli hiyo wamesema Mafunzo hayo yatawasaidia kuengeza ujuzi katika Masomo yao na kutokua tegemezi wanapokuwa katika Jamii.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.