MKOA WA LINDI UMEPOKEA TRILIONI 1.2 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO

MKUU WA MKOA WA LINDI

Mkoa wa Lindi umepokea Jumla ya Shilingi Tilioni 1.2 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Elimu, Afya, Maji Umeme Barabara na huduma nyingine kwa Kipindi cha Mwezi March 2021 hadi March 2024

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack alipokuwa akizungumza na Wafanyakazi na Wananchi wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika huko Wilayani Ruangwa 

Amesema  amesema Mafanikio hayo yametokana na utendaji kazi mzuri wa Watumishi huku akibainisha kuwa nchi zote zilizopiga hatua ya maendelea Ulimwenguni zilitokana na uwajibikaji na utendaji kazi kwa Watumishi katika Sekta mbalimbali 

Amewapongeza Watumishi kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii licha ya matatizo mbalimbali huku Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi  Banarbas Esau akieleza namna chama kinavyolidhishwa na utendaji kazi wa Watumishi katika utekelezaji wa Ilani

Awali mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Ruangwa akaelezea umuhimu wa  Siku hiyo ya Wafanyakazi 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.