JENERALI MABEYO AWAVISHA VYEO MAKAMISHNA WAPYA NCAA

Makamishna NCAA

    Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu)  amewavisha vyeo maafisa Uhifadhi wakuu waliopandishwa vyeo hivi karibuni katika tukio lililofanyika ofisi za Makao makuu ya NCAA Karatu Mkoani Arusha.

      Waliovishwa vyeo ni Afisa Uhifadhi Mkuu Lilian Magoma ambae amepandishwa na kuvishwa cheo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia idara ya Mipango, tathmini na ufuatiliajI na Afisa Uhifadhi Mwandamizi wa Rasilimali watu Salma Chisonga aliyepandishwa cheo  amevishwa cheo kuwa Kamishna msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi, Rasilimali watu na Utawala.

     Jenerali Mabeyo amewataka makamishna wapya kufanya kazi kwa kujituma na kuzingatia viapo vyao katika misingi ya uzalendo, maadili ya utumishi, ushirikiano, maarifa na bidii ya kazi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.