DKT.MWINYI AWASILI PEMBA KWA ZIARA YA KIKAZI

Dkt.Mwinyi akiwasili Pemba

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili uwanja wa ndege wa Pemba kwa ziara ya kikazi

     Dk. Mwinyi amepokelewa na Wakuu wa Mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba, Mhe. Mattar Zahor Masoud na Salama  Mbarouk Khatibu, viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, leo tarehe 30 Aprili 2024.

     Rais Dk. Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za siku ya wafanyakazi duniani  (Mei Mosi) ambapo kwa Zanzibar  zitafanyika Uwanja wa Gombani, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa  kusini Pemba

     Akiwa ziarani kisiwani Pemba Rais Dk. Mwinyi pia atafungua Skuli ya ghorofa ya Sekondari, Utaani Wilaya ya  Wete Mkoa wa Kaskazini, Pemba.

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.