MAFURIKO YAATHIRI NYUMBA 32 NA MASHAMBA KILOSA

MAFURIKO KILOSA
English

Nyumba 32 zimeathiriwa na mafuriko huku Nyumba Sita zikibomoka kabisa  pamoja na Mashamba yenye Mazao mbalimbali yakiwemo Mahindi ekari 300 yamesombwa na maji ya mafuriko katika Kijiji cha Mhenda kilichopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali Wilayani humo.

‎Akizungumza na ZBC juu ya  athari  hizo za mvua hizo ambazo zimenyesha Usiku wa kuamkia Machi 13 Mwaka huu Mwenyekiti wa Kijiji cha Mhenda kilichopo Wilaya ya Kilosa Chande Abdallah  amesema kutokana na athari hizo ameushukuru uongozi wa Wilaya ya Kilosa ukiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Shaka Hamdu Shaka kwa kutuma kitengo Cha maafa kufika kwenye Kijiji hicho na kuchukua taarifa za athari za mafuriko Ili kuangalia namna ya kuwasaidia wananchi.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.